Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Abna likimnukuu Al-Mayadeen, vyanzo vya ndani vimeripoti kwamba doria ya vikosi vya kikalia vya Kizayuni yenye wanajeshi 60 na magari 15 ya kivita, leo asubuhi ilivamia kijiji cha "Ufaniya" katika vitongoji vya kaskazini mwa Quneitra kusini mwa Syria.
Vyanzo vya ndani vya Syria vimetangaza kwamba doria hii ya Israeli ilifunga njia za kuingia kijijini na kuanzisha kituo cha ukaguzi kwenye barabara inayounganisha kijiji cha Ufaniya na mji wa Jabata al-Khashab.
Wakalia wa Kizayuni jana pia walivamia barabara inayounganisha miji ya al-Muallaqa na Ghadir al-Bustan katika vitongoji vya Quneitra na kuanzisha kituo cha ukaguzi.
Zaidi ya wiki moja iliyopita, vikosi vya kikalia vya Kizayuni vilivamia bwawa la al-Muntara katika vitongoji vya kati vya Quneitra.
Uvamizi huu wa Israel katika mfumo wa mashambulizi yanayoendelea dhidi ya uhuru na ardhi ya Syria na usalama wa raia wake umeongezeka tangu anguko la Bashar al-Assad mnamo Desemba 8, 2024. Zaidi ya uvamizi huu umejikita katika mkoa wa Quneitra na vitongoji vyake kusini mwa nchi hiyo.
Your Comment